bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Hosea 7
Hosea 7
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
1
Kila mara nikitaka kurudishia watu wangu hali yao ya mbele, ninapotaka kuwaponyesha Waisraeli, uovu wa watu wa Efuraimu unafunuliwa, matendo mabaya ya Samaria yanajitokeza. Wao wanaongozwa na udanganyifu, mwizi anabomoa nyumba; inje katika barabara wanyanganyi wanashambulia.
2
Hawafikiri hata kidogo kwamba mimi ninayakumbuka maovu yao yote. Sasa maovu yao yamewabana. Yote waliyotenda yako mbele yangu.
3
Wanamufurahisha mufalme, lakini ni waovu; wanawafurahisha wakubwa, lakini ni wanafiki.
4
Wote ni wazinzi; wao ni kama furu iliyowashwa moto ambayo mutengenezaji wa mikate haichochei tangia wakati anapoponda unga mpaka mikate itakapovimba.
5
Kwenye sikukuu ya mufalme, waliwalewesha sana wakubwa wake; naye mufalme akashirikiana na watu wa ovyoovyo.
6
Kama vile furu inavyowaka ndivyo mioyo yao inavyowaka kwa udanganyifu; usiku kucha hasira yao inafukiza moshi, inapofika asubui, inawaka kama ndimi za moto.
7
Wote wamewaka hasira kama furu, na wanawaangamiza watawala wao. Wafalme wao wote wameanguka, wala hakuna anayeniomba musaada.
8
Efuraimu amechanganika na watu wa mataifa. Anaonekana kama mukate ambao haukugeuzwa.
9
Wageni wamenyonya nguvu zake, wala yeye mwenyewe hajui; imvi zimejaa juu ya kichwa chake, lakini yeye mwenyewe hana habari.
10
Kiburi cha Waisraeli kinawashuhudia wao wenyewe, hawanirudilii mimi Yawe, Mungu wao; wala hawanitafuti kwa ajili ya matukio hayo yote.
11
Efuraimu ni kama njiwa mujinga asiyekuwa na akili; mara yuko Misri, mara Asuria kwa kuomba musaada.
12
Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege toka katika anga; nitamwaazibu kufuatana na jinsi walivyotangaza kwa kusanyiko lao.
13
Ole kwao kwa sababu wameniacha! Maangamizi yawapate, maana wameniasi. Nilitaka kuwakomboa, lakini wanasema uongo juu yangu.
14
Wananililia, lakini si kwa moyo. Wanagaagaa na kujikatakata juu ya vitanda vyao, kusudi nisikilize maombi yao kwa kupata ngano na divai; lakini wanaendelea kuniasi.
15
Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao, lakini wanafikiri maovu juu yangu.
16
Wanaigeukia miungu ya bure, wako kama upinde ulioregea. Waongozi wao watakufa kwa upanga, kwa sababu ya maneno yao ya kiburi. Kwa hiyo, watazarauliwa katika inchi ya Misri.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14