bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Isaiah 42
Isaiah 42
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 43 →
1
Muangalie mutumishi wangu ninayemusaidia; muchaguliwa wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye ataimarisha sheria yangu katika mataifa.
2
Hatalalamika wala hatapiga kelele, wala hatasema kwa sauti kubwa katika barabara.
3
Hatavunja tete lililokunjama, hatazimisha utambi unaotoa moshi; ataimarisha sheria yangu kwa uaminifu.
4
Yeye hataregea wala kuchoka, mpaka atakapoimarisha sheria yangu katika dunia. Watu wa mbali wanangojea mafundisho yake.
5
Hivi ndivyo anavyosema Yawe aliyeumba mbingu na kuzitandika kama hema, aliyeifanya dunia na vyote vinavyokuwa ndani yake, anayewapa watu wanaokaa ndani yake uzima, na kuwajalia uzima wote wanaoishi ndani yake:
6
Mimi Yawe nimekuita kutenda haki, nimekushika mukono na kukulinda. Kwa njia yako nitafanya ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwangaza wa mataifa.
7
Utayafungua macho ya vipofu, utawafungua wafungwa toka katika kifungo, utawaweka huru wale waliofungwa katika giza.
8
Jina langu mimi ni Yawe; sitamupa mwingine utukufu wangu, wala sifa zangu sanamu za miungu.
9
Mambo niliyotabiri yametukia; na sasa ninatangaza mambo mapya, ninakuelezea hayo mbele hayajatukia.
10
Mumwimbie Yawe wimbo mupya! Dunia yote iimbe sifa zake: bahari na vyote vinavyokuwa ndani yake, inchi za mbali na wakaaji wake;
11
jangwa na miji yake yote vipige kelele, vijiji vya wakaaji wa Kedari vimusifu, wakaaji wa Sela waimbe kwa shangwe; wapige kelele kutoka juu kwenye mulima.
12
Wote wanaokaa katika inchi za mbali, wamutukuze na kumusifu Yawe.
13
Yawe anajitokeza kama shujaa; kama vile askari katika vita anatatanua kupigana. Anapiga kelele kubwa la vita na kujionyesha mwenye nguvu juu ya waadui zake.
14
Yawe anasema hivi: Kwa muda murefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuiza; lakini sasa nitalia kama mwanamuke wakati wa kuzaa, anayeugua pamoja na kupumua kwa nguvu.
15
Nitaharibu milima na vilima, na majani yote nitayakausha. Mito ya maji nitaigeuza kuwa inchi kavu, na visima vya maji nitavikausha.
16
Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao nitaligeuza giza kuwa mwangaza, na pahali penye kuharibika patakuwa laini. Huo ndio mupango wangu wa kufanya, nami nitautimiza.
17
Wote wanaotegemea sanamu za miungu, wote wanaoziambia “Ninyi ni miungu yetu” watakomeshwa na kupata haya.
18
Musikilize enyi viziwi! Muangalie, enyi vipofu, mupate kuona!
19
Nani anayekuwa kipofu isipokuwa mutumishi wangu? Nani anayekuwa kiziwi kama mujumbe ninayemutuma? Ni nani anayekuwa kipofu kama huyu niliyemutakasa, au kipofu kama mutumishi wa Yawe?
20
Ninyi mumeona mambo mengi, lakini hamuelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamusikii kitu!
21
Kwa ajili ya uaminifu wake, Yawe, alipenda kutukuza sheria yake na kuiheshimisha.
22
Lakini hawa ni watu walioibwa mali yao na kunyanganywa! Wote wamenaswa katika mashimo, wamefungwa katika kifungo. Wamenyanganywa bila mutu wa kuwaokoa, wamekamatwa mateka na hakuna anayesema: Muwarudishe!
23
Mutatega masikio kwa kusikia kitu hiki? Nani kati yenu atakayesikiliza vizuri yatakayotukia?
24
Ni nani aliyewatia Waisraeli katika mikono ya waadui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Yawe ambaye tumemukosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.
25
Kwa hiyo aliwamwangia kasirani yake kali, akawaacha kupatwa na vita kali. Hasira yake iliwawakia kila upande, lakini wao hawakuelewa chochote; iliwachoma, lakini hawakufikiri juu ya jambo hilo.
← Chapter 41
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 43 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66