bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Job 39
Job 39
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
1
Unajua mbuzi wa milima anazaa wakati gani, au umekwisha kuona kulungu akizaa?
2
Unajua anapata mimba kwa muda gani, au siku yenyewe ya kuzaa unaijua?
3
Wanachutama kwa kuzaa, wanazaa vitoto vyao.
4
Vitoto vyao vinapata nguvu, vinakomaa kulekule katika pori, kisha vinawaacha wamama zao na kwenda zao.
5
Nani aliyemwacha huru punda wa pori? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?
6
Mimi niliwapa jangwa likuwe nyumba yao, mbuga zenye chumvi kuwa makao yao.
7
Wanajitenga kabisa na makelele ya miji, hawasikilizi kelele la muchungaji.
8
Wanatembeatembea katika milima kwa kupata malisho, na kutafuta kitu chochote kinachokuwa kibichi.
9
Mbogo atakubali kukutumikia? Atakubali kulala katika zizi lako?
10
Unaweza kumufunga mbogo kamba kwa kulima shamba, au akokote jembe la kulima?
11
Utamutegemea kwa sababu ana nguvu nyingi na kumwacha akufanyie kazi zako nzito?
12
Unamutazamia mbogo akuvunie mavuno yako, na kuleta ngano kwenye nafasi ya kupepetea?
13
Mbuni anapigapiga mabawa yake kwa furaha, lakini hawezi kuruka kama korongo.
14
Mbuni anayaacha mayai yake juu ya udongo kusudi yapate joto ndani ya muchanga;
15
lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa, au kuvunjwa na nyama wa pori.
16
Mbuni anatendea vitoto vyake kwa ukali kama vile si vyake, hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi;
17
kwa sababu nilimufanya asahau hekima yake, wala sikumupa sehemu yoyote ya akili.
18
Lakini akianza kukimbia, anamuchekelea hata farasi na mupanda-farasi.
19
Yobu, ni wewe ndiwe uliyewapa farasi nguvu, ukawavalisha kwenye shingo manyoya marefu?
20
Ni wewe unayemufanya farasi aruke kama nzige? Mulio wake wa maringo ni wa ajabu!
21
Anakwaruzakwaruza udongo katika mabonde kwa pupa; anakimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.
22
Farasi anaichekelea hofu, na hatishiki; wala upanga hauwezi kumurudisha nyuma.
23
Silaha wapanda-farasi wanazobeba, zinagongana kwa sauti na kuangaa kwenye jua.
24
Farasi anasonga mbele, akitetemeka kwa hasira; baragumu inapolia, yeye hasimami.
25
Kila mara baragumu inapopigwa, yeye anatoa sauti; anasikia harufu ya vita toka mbali, anasikia mushindo wa majemadari wakitoa amri kwa makelele.
26
Mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka, na kunyoosha mabawa yake kuelekea upande wa kusini?
27
Tai anapanda juu kwa amri yako, na kuweka chicha yake juu kwenye milima?
28
Tai anafanya makao yake juu ya mawe marefu, na incha kali za mawe makubwa ndizo maficho yake.
29
Kutoka kule anavizia nyama, macho yake yanaiona kutoka mbali.
30
Vitoto vyake vinafyonza damu; pale muzoga unapokuwa ndipo tai anapokuwa.
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42