1 Kings 12:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: ‘Msiende, wala msipigane na ndugu zenu, watu wa Israeli. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni mpango wangu.’” Basi, wakaufuata ujumbe huu wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani tena, kama Mwenyezi-Mungu alivyoagiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Mwenyezi Mungu na kurudi nyumbani, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la Bwana, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: ‘Msiende, wala msipigane na ndugu zenu, watu wa Israeli. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni mpango wangu.’” Basi, wakaufuata ujumbe huu wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani tena, kama Mwenyezi-Mungu alivyoagiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Hili ndilo asemalo BWANA: Usipande kupigana dhidi ya ndugu zako, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili limetoka kwangu.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la BWANA na kurudi nyumbani, kama BWANA alivyokuwa ameagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Hili ndilo asemalo bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la bwana na kurudi nyumbani, kama bwana alivyokuwa ameagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la BWANA, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: ‘Msiende, wala msipigane na ndugu zenu, watu wa Israeli. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni mpango wangu.’” Basi, wakaufuata ujumbe huu wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani tena, kama Mwenyezi-Mungu alivyoagiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Msipande kwenda kupigana na ndugu zenu, wana wa Isiraeli! Rudini kila mtu nyumbani kwake! Kwani jambo hili limefanywa na mimi. Walipolisikia neno hili la Bwana, wakarudi kwenda zao, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la BWANA, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwamba mimi Yawe ninasema hivi: ‘Musiende, wala musipigane na wandugu zenu, watu wa Israeli. Murudie kila mutu kwake, maana hayo yaliyotokea ni mupango wangu.’ ” Basi, wakaufuata ujumbe huu wa Yawe, wakarudi kwao tena kama vile Yawe alivyoagiza.