Ezra 8:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa koo za watu waliorudi pamoja nami Ezra kutoka Babuloni, wakati wa utawala wa mfalme Artashasta:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao, na hii ndiyo nasaba ya wale waliokwea pamoja nami kutoka Babeli, wakati wa kutawala kwake mfalme Artashasta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa koo za watu waliorudi pamoja nami Ezra kutoka Babuloni, wakati wa utawala wa mfalme Artashasta:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hawa ndio wakuu wa koo za baba zao, na hii ndiyo nasaba ya wale waliokwea pamoja nami kutoka Babeli, wakati wa kutawala kwake mfalme Artashasta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa koo za watu waliorudi pamoja nami Ezra kutoka Babuloni, wakati wa utawala wa mfalme Artashasta:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa ndio wakuu wa milango ya baba zao na hesabu ya vizazi vyao waliopanda na mimi kutoka Babeli katika siku za ufalme wa mfalme Artasasta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao, na hii ndiyo nasaba ya wale waliokwea pamoja nami kutoka Babeli, wakati wa kutawala kwake mfalme Artashasta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hayo ndiyo majina ya viongozi wa ukoo za watu waliorudi pamoja nami Ezra kutoka Babeli, wakati wa utawala wa mufalme Artasasta: Gersomi, wa ukoo wa Finehasi; Danieli, wa ukoo wa Itamari; Hatusi, wa ukoo wa Daudi; mwana mumoja wa ukoo wa Sekania; Zakaria, wa ukoo wa Parosi, pamoja na wanaume mia moja na makumi tano wa ukoo wake, walioandikishwa pamoja; Eliyoenayi mwana wa Zerahia, wa ukoo wa Pahati-Moabu, pamoja na wanaume mia mbili; Sekania mwana wa Yahasieli, wa ukoo wa Zatu, pamoja na wanaume mia tatu; Ebedi mwana wa Yonatani, wa ukoo wa Adini, pamoja na wanaume makumi tano; Yesaya mwana wa Atalia, wa ukoo wa Elamu, pamoja na wanaume makumi saba; Zebadia mwana wa Mikaeli, wa ukoo wa Sefatia, pamoja na wanaume makumi nane; Obadia mwana wa Yehieli, wa ukoo wa Yoabu, pamoja na wanaume mia mbili kumi na wanane; Selemoti mwana wa Yosifia, wa ukoo wa Bani, pamoja na wanaume mia moja na makumi sita; Zakaria mwana wa Bebayi, wa ukoo wa Bebayi, pamoja na wanaume makumi mbili na wanane; Yohanani mwana wa Hakatani, wa ukoo wa Azgadi, pamoja na watu mia moja na kumi; Elifeleti, Yueli na Semaya, wa ukoo wa Adonikamu, pamoja na wanaume makumi sita, (hawa walirudi kisha); Utayi na Zakuri, wa ukoo wa Bigwayi pamoja na wanaume makumi sita.