bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
2 Chronicles 5
2 Chronicles 5
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
1
Hivyo, Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote Daudi baba yake aliyokuwa ameiweka wakfu, yaani: Fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu.
2
Basi mfalme Solomoni akawakutanisha Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.
3
Ndipo wote walipokutana mbele ya mfalme katika sikukuu ya mwezi wa saba.
4
Baada ya wazee wote wa Israeli kuwasili, Walawi walilibeba sanduku la agano,
5
Walawi na makuhani walilihamisha sanduku la agano na hema la mkutano na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa humo hemani.
6
Mfalme Solomoni na mkutano wa Israeli wakakusanyika mbele ya sanduku la agano nao wakatoa sadaka za ng'ombe na kondoo wasiohesabika.
7
Kisha makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, mahali patakatifu sana, chini ya mabawa ya wale viumbe.
8
Hao viumbe wenye mabawa walitandaza mabawa yao juu ya mahali lilipowekwa sanduku, kwa hiyo sanduku na mipiko yake ya kulibebea vilikuwa chini ya mabawa.
9
Kwa kuwa mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana, ncha zake ziliweza kuonekana kutoka mahali patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa nje. Mipiko hiyo ingali mahali hapo hata leo.
10
Hakukuwa na kitu ndani ya sanduku la agano, ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri.
11
Ikawa makuhani walipotoka pale mahali patakatifu, (kwa sababu makuhani wote waliokuwapo bila kujali makundi yao, walikuwa wamejitakasa.),
12
Walawi wote waimbaji, wakiwamo Asafu, Hemani, na Yeduthuni, pamoja na Walawi wengine wa koo zao, wakiwa wamejivalia nguo zao za kitani safi huku wamebeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu. Makuhani 120 wapiga tarumbeta walikuwa pamoja nao.
13
Waimbaji, huku wakifuatiwa na sauti linganifu za tarumbeta, matoazi na vyombo vingine vya muziki, walimsifu Mwenyezi-Mungu wakiimba: “Maana yeye ni mwema, na fadhili zake zadumu milele.” Wakati huo nyumba ya Mwenyezi-Mungu ilijazwa wingu.
14
Nao makuhani walishindwa kuhudumu humo kwa sababu ya wingu hilo, maana utukufu wa Mwenyezi-Mungu uliijaza nyumba ya Mungu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36