bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Ezekiel 19
Ezekiel 19
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 20 →
1
Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli:
2
Mama yenu alikuwa simba wa fahari miongoni mwa simba wengine. Alikaa kati ya simba vijana, akawalisha watoto wake.
3
Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake, mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari. Akajifunza kwa mama yake kuwinda, akawa simba mla watu.
4
Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake, wakamnasa katika mtego wao, wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.
5
Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja, matumaini ya kumpata yamekwisha, alimchukua mtoto wake mwingine, akamfanya simba kijana hodari.
6
Huyo alipokuwa amekua, akaanza kuzurura na simba wengine. Naye pia akajifunza kuwinda, akawa simba mla watu.
7
Aliziandama ngome za watu na kuiharibu miji yao. Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake, kwa sauti ya kunguruma kwake.
8
Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote, wakatandaza wavu wao juu yake, naye akanaswa katika mtego wao.
9
Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao, wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni. Huko, wakamtia gerezani, ili ngurumo yake isisikike tena juu ya milima ya Israeli.
10
Mama yako alikuwa kama mzabibu shambani, uliopandikizwa kando ya maji, ambao ulizaa sana kwa kuwa na maji tele.
11
Ulikuwa na matawi yenye nguvu, ambayo yalikuwa fimbo za kifalme. Mzabibu huo ulikua kupita miti mingine, watu waliusifu ukubwa wa shina lake na wingi wa matawi yake.
12
Lakini ulingolewa kwa hasira ukatupwa chini ardhini; upepo wa mashariki ukaukausha, matunda yake yakapukutika; matawi yake yenye nguvu yalikaushwa, nao moto ukauteketeza.
13
Na sasa umepandikizwa jangwani, katika nchi kame isiyo na maji.
14
Lakini moto umetoka kwenye shina lake, umeyateketeza matawi na matunda yake. Matawi yake kamwe hayatakuwa na nguvu, wala hayatakuwa fimbo za kifalme. Huo umekuwa wimbo wa maombolezo; ndivyo unavyoimbwa daima.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48