bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Numbers 24
Numbers 24
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
1
Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani.
2
Alitazama juu akawaona Waisraeli wamepiga kambi, kila kabila mahali pake. Kisha roho ya Mungu ikamjia,
3
naye akatamka kauli hii ya kinabii: Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peori kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho;
4
kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu, mtu anayesujudu na kuona wazi.
5
Hema zako zapendeza namna gani enyi watu wa Yakobo; naam, kambi zenu enyi watu wa Israeli!
6
Ni kama mabonde yanayotiririka maji, kama bustani kandokando ya mto, kama mishubiri aliyopanda Mwenyezi-Mungu, kama mierezi kandokando ya maji.
7
Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji, mbegu yao itapata maji mengi, mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi, na ufalme wake utatukuka sana.
8
Mungu aliwachukua kutoka Misri, naye huwapigania kwa nguvu kama nyati. Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao, atavunjavunja mifupa yao, atawachoma kwa mishale yake.
9
Ataotea na kulala chini kama simba, nani atathubutu kumwamsha? Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli, alaaniwe yeyote atakayewalaani.
10
Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki!
11
Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”
12
Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu
13
kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14
“Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.”
15
Basi, Balaamu akatamka kauli hii: “Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori, kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16
kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu, na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu, mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu, mtu anayesujudu, macho wazi.
17
Ninamwona, atakayekuja, lakini baadaye, namwona, lakini hayuko karibu. Nyota itatokea kwa wazawa wa Yakobo, atatokea mfalme miongoni mwa Waisraeli. Kwa fimbo yake atawachapa viongozi wa Wamoabu atawaangamiza wazawa wote wa Sethi.
18
Edomu itamilikiwa naye, Seiri itakuwa mali yake, Israeli itapata ushindi mkubwa.
19
Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.”
20
Kisha Balaamu akawaangalia Waamaleki, akatoa kauli hii: “Amaleki ni taifa lenye nguvu kuliko yote, lakini mwishoni litaangamia kabisa.”
21
Kisha Balaamu akawaangalia Wakeni, akatoa kauli hii: “Makao yenu ni salama, enyi Wakeni, kama kiota juu kabisa mwambani.
22
Lakini mtateketezwa, enyi Wakeni. Mtachukuliwa mateka na Ashuru mpaka lini?”
23
Tena Balaamu akatoa kauli hii: “Lo! Nani ataishi, Mungu atakapofanya hayo?
24
Meli zitafika kutoka Kitimu, wataishambulia Ashuru na Eberi, lakini nao pia wataangamia milele.”
25
Basi, Balaamu akaondoka, akarudi nyumbani; Balaki pia akaenda zake.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36