bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
/
Hebrews 5
Hebrews 5
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
1
Kila kuhani Mkuu wa Kiyahudi alichaguliwa kutoka miongoni mwa watu. Kuhani huyo anapewa kazi ya kuwasaidia watu katika mambo wanayopaswa kumfanyia Mungu. Anapaswa kumtolea Mungu sadaka na sadaka za dhambi.
2
Kuhani mkuu anao udhaifu wake binafsi. Hivyo anapaswa kuwa mpole kwa wale wanaokosea kwa sababu ya kutokujua.
3
Hutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zao, lakini kutokana na udhaifu wake anapaswa pia kutoa sadaka kwa ajili dhambi zake mwenyewe.
4
Kuwa kuhani mkuu ni heshima. Lakini hayupo anayejichagua mwenyewe kwa ajili ya kazi hii. Mtu huyo anapaswa kuwa amechaguliwa na Mungu kama alivyokuwa Haruni.
5
Ndivyo ilivyo hata kwa Kristo. Hakujichagua mwenyewe kuwa na heshima na kuwa kuhani mkuu. Lakini Mungu alimchagua. Mungu akamwambia: “Wewe ni mwanangu. Leo nimekuwa baba yako.”
6
Na katika sehemu nyingine ya Maandiko Mungu anasema: “Wewe ni kuhani mkuu milele; kama Melkizedeki alivyokuwa kuhani.”
7
Yesu alipoishi duniani alimwomba Mungu, akiusihi msaada kutoka kwa yule anayeweza kumwokoa kutoka mauti. Alimwomba Mungu kwa sauti kuu na kwa machozi. Na Mungu alizisikia sala zake kwa sababu ya heshima yake kuu kwa Mungu.
8
Yesu alikuwa mwana wa Mungu, lakini aliteseka, na kwa njia ya mateso yake alijifunza kutii chochote alichosema Mungu.
9
Hili lilimfanya yeye awe kuhani mkuu mkamilifu, anayetoa njia kwa ajili ya kila mmoja anayemtii ili kuokolewa milele.
10
Mungu alimfanya yeye kuhani mkuu, kama alivyokuwa Melkizedeki.
11
Tunayo mambo mengi ya kuwaeleza kuhusu hili. Lakini ni vigumu kufafanua kwa sababu mmeoteza shauku ya kusikiliza.
12
Mmekuwa na muda wa kutosha ambapo sasa mngepaswa kuwa walimu. Lakini mnahitaji mtu awafundishe tena mafundisho ya Mungu ya mwanzo. Bado mnahitaji mafundisho ambayo yako kama maziwa. Hamjafikia kiwango cha chakula kigumu.
13
Yeyote anayeishi kwa kutegemea maziwa tu bado ni mtoto mchanga, hayupo tayari kuelewa zaidi kuhusu kuishi kwa haki.
14
Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu ambao wamekua. Kutokana na uzoefu wao wamejifunza kuona tofauti baina ya jema na ovu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13