bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
1 Corinthians 5
1 Corinthians 5
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 6 →
1
Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujafanyika hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake.
2
Nanyi mwajivuna! Je, haiwapasi kuhuzunika na kumtenga na ushirika wenu mtu huyo aliyefanya mambo hayo?
3
Hata kama siko pamoja nanyi katika mwili, niko nanyi katika roho. Nami nimekwisha kumhukumu mtu huyo aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwepo.
4
Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Isa nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho, na uweza wa Bwana Isa ukiwepo,
5
mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, lakini roho yake iokolewe katika siku ya Mwenyezi Mungu.
6
Majivuno yenu si mazuri. Je, hamjui kwamba chachu kidogo huchachusha donge zima la unga?
7
Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Al-Masihi, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu.
8
Kwa hiyo, tusiiadhimishe sikukuu hii kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, ndio weupe wa moyo na kweli.
9
Niliwaandikia katika waraka wangu kuwa msishirikiane na wazinzi.
10
Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu.
11
Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye.
12
Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kundi la waumini? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani?
13
Mungu atawahukumu hao walio nje. “Ninyi mwondoeni huyo mtu mwovu miongoni mwenu.”
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16