bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
2 Chronicles 3
2 Chronicles 3
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
1
Ndipo Sulemani akaanza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Mwenyezi Mungu alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi.
2
Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.
3
Msingi aliouweka Sulemani kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa na urefu wa dhiraa sitini, na upana wa dhiraa ishirini kwa kipimo cha kale.
4
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo, na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
5
Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za msunobari, na kufunikwa kwa dhahabu safi, na kuupamba kwa michoro ya mitende na minyororo.
6
Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu.
7
Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta.
8
Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 600 za dhahabu safi.
9
Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.
10
Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu.
11
Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu; bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi mwingine.
12
Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu, na bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza.
13
Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa.
14
Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake.
15
Mbele ya Hekalu Sulemani akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na urefu wa dhiraa thelathini na tano kwenda juu, na kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye kimo cha dhiraa tano.
16
Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga mia moja, na kuyaunganisha kwenye minyororo.
17
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36