bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Isaiah 2
Isaiah 2
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 3 →
1
Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:
2
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Mwenyezi Mungu utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko.
3
Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni kwenye mlima wa Mwenyezi Mungu, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Torati itatoka Sayuni, neno la Mwenyezi Mungu litatoka Yerusalemu.
4
Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.
5
Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Mwenyezi Mungu.
6
Mwenyezi Mungu umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina unaotoka Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
7
Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao ya vita.
8
Nchi yao imejaa sanamu; wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.
9
Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.
10
Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa enzi yake!
11
Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.
12
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),
13
kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,
14
kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,
15
kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,
16
kwa kila meli ya biashara, na kila mashua ya kifahari.
17
Majivuno ya mwanadamu yatashushwa, na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
18
nazo sanamu zitatoweka kabisa.
19
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
20
Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
21
Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
22
Acheni kumtumainia mwanadamu, ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake. Yeye ana thamani gani?
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66