bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
/
Leviticus 17
Leviticus 17
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 18 →
1
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,
2
“Sema na Haruni na wanawe, pamoja na Waisraeli wote, uwaambie: ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloagiza:
3
Mwisraeli yeyote atakayetoa dhabihu ya ng’ombe, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake,
4
badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu mbele ya Maskani ya Mwenyezi Mungu, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu, na ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
5
Hii ni ili Waisraeli wamletee Mwenyezi Mungu dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Mwenyezi Mungu, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kuwa sadaka za amani.
6
Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Mwenyezi Mungu katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
7
Kamwe wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa vizazi vijavyo.’
8
“Waambie: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu
9
bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
10
“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakula damu yoyote, nitakuwa kinyume chake, na nitamkatilia mbali na watu wake.
11
Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu.
12
Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kula damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kula damu.”
13
“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo,
14
kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msile damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali.”
15
“ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni; kisha atakuwa ametakaswa.
16
Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ”
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27