bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Amos 9
Amos 9
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
1
Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga juu ya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote, na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna awaye yote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka.
2
Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha.
3
Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, huko nitawawinda na kuwakamata. Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu katika vilindi vya bahari, huko nako nitaamuru joka kuwauma.
4
Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, huko nako nitaamuru upanga uwaue. Nitawakazia macho yangu kwa mabaya wala si kwa mazuri.”
5
Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Nile, kisha hushuka kama mto wa Misri;
6
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: BWANA ndilo jina lake.
7
“Je, Waisraeli, ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” asema BWANA. “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, Wafilisti toka Kaftori na Washami kutoka Kiri?
8
“Hakika macho ya BWANA Mwenyezi yako juu ya ufalme wenye dhambi. Nami nitauangamiza kutoka kwenye uso wa dunia: hata hivyo sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo,” asema BWANA.
9
“Kwa kuwa nitatoa amri, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo, na hakuna hata punje moja nzuri itakayoanguka chini.
10
Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu watauawa kwa upanga, wale wote wasemao, ‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’
11
“Katika siku ile nitaisimamisha hema ya Daudi iliyoanguka. Nitakarabati mahali palipobomoka na kujenga upya magofu yake, na kujenga kama ilivyokuwa awali,
12
ili wapate kumiliki mabaki ya Edomu na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,” asema BWANA ambaye atafanya mambo haya.
13
“Siku zinakuja,” asema BWANA, “wakati mvunaji atakapotanguliwa na mkulima na mpanzi atakapotanguliwa na yeye akamuaye zabibu. Divai mpya itadondoka kutoka milimani na kutiririka kutoka vilima vyote.
14
Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, nao wataishi ndani mwake. Watapanda mizabibu na kunywa divai yake, watalima bustani na kula matunda yake.
15
Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe, hawatang'olewa tena kutoka katika nchi ambayo nimewapa,” asema BWANA Mungu wenu.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9