bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Deuteronomy 27
Deuteronomy 27
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 28 →
1
Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo.
2
Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo BWANA Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu.
3
Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo BWANA Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile BWANA, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.
4
Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu.
5
Huko mjengeeni BWANA Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa cho chote cha chuma juu yake.
6
Jengeni madhabahu ya BWANA Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa BWANA Mungu wenu.
7
Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za BWANA Mungu wenu.
8
Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.”
9
Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza Ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la BWANA Mungu wako.
10
Mtii BWANA Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”
11
Siku ile ile Mose akawaagiza watu:
12
Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini.
13
Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.
14
Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15
“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
16
“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
17
“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
18
“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
19
“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
20
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
21
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama ye yote.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
22
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
23
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
24
“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
25
“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumwua mtu asiye na hatia.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
26
“Alaaniwe mtu ambaye hatashika maneno haya ya sheria hii kwa kuyafanya.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34