bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Lamentations 4
Lamentations 4
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
1
Jinsi dhahabu ilivyopoteza mng'ao wake, dhahabu iliyo safi imekuwa haing'ai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara.
2
Jinsi wana wa Sayuni wenye thamani, ambao mwanzo uzito wa thamani yao ulikuwa wa dhahabu, sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo, kazi ya mikono ya mfinyanzi!
3
Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni katika jangwa.
4
Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga umegandamana na kaakaa la kinywa chake, watoto huomba mkate, lakini hakuna ye yote awapaye.
5
Wale waliokula vyakula vya kifahari ni maskini barabarani. Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau sasa wanalala kwenye malundo ya majivu.
6
Adhabu ya watu wangu ni kubwa kuliko ile ya Sodoma, ambayo ilipinduliwa ghafula bila kuwepo mkono wa kumsaidia.
7
Wakuu wao walikuwa wameng'aa kuliko theluji na weupe kuliko maziwa, miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, kuonekana kwao kama yakuti samawi.
8
Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; hawatambulikani barabarani. Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, imekuwa mikavu kama fimbo.
9
Wale waliouawa kwa upanga ni bora kuliko wale waliokufa kwa njaa; waliteseka kwa njaa, walitokomea kwa ajili ya kukosa chakula kutoka shambani.
10
Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma walipika watoto wao wenyewe, ambao walikuwa chakula chao wakati watu wangu walipoangamizwa.
11
BWANA ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake; ameimwaga hasira yake kali. Amewasha moto katika Sayuni ambao umeteketeza misingi yake.
12
Wafalme wa dunia hawakuamini, wala hapakuwepo mtu ye yote wa duniani, kwamba adui na watesi wangeweza kuingia kwenye malango ya Yerusalemu.
13
Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake, na maovu ya makuhani wake, ambao walimwaga pamoja naye damu ya wenye haki.
14
Sasa wanapapasa papasa barabarani kama watu ambao ni vipofu. Wamenajisiwa kabisa kwa damu kwamba hakuna ye yote anayethubutu kugusa mavazi yao.
15
Watu waliwapigia kelele wakisema, “Ondokeni! Ninyi ni najisi! Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!” Walipokimbia na kutangatanga huko na huko, watu miongoni mwa mataifa walisema, “Hawawezi kukaa hapa zaidi.”
16
BWANA mwenyewe amewatawanya; hawaangalii tena. Makuhani hawaonyeshwi heshima, wazee hawakubaliki.
17
Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka, kwa kutazamia bure msaada; tuliangalia kutoka minara yetu kwa taifa lile lisiloweza kutuokoa.
18
Watu walitunyemelea katika kila hatua kwa hiyo hatukuweza kutembea katika barabara zetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia, kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika.
19
Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai katika anga; walitusaka juu milimani na kutuvizia jangwani.
20
Mpakwa mafuta wa BWANA, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.
21
Shangilia na ufurahi, Ee Binti Edomu, wewe ambaye unaishi katika nchi ya Usi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa, Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.
22
Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha, hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni. Lakini, Ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako na atafunua uovu wako.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5