bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Nehemiah 7
Nehemiah 7
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
1
Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na kuweka milango, waliteuliwa mabawabu wa lango, waimbaji na Walawi.
2
Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.
3
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Wakati walinzi wa malango wakiwa kwenye zamu, wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
4
Mji ulikuwa mkubwa tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.
5
Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi iliyoandikwa ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6
Hawa ndio watu wa jimbo waliorudi kutoka utumwani uhamishoni walikokuwa wamepelekwa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
7
wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana): Orodha ya watu wa Israeli:
8
wazao wa Paroshi — 2,172
9
wazao wa Shefatia — 372
10
wazao wa Ara — 652
11
wazao wa Pahath-Moabu (kupitia ukoo wa Yeshua na Yoabu) — 2,818
12
wazao wa Elamu — 1,254
13
wazao wa Zatu — 845
14
wazao wa Zakai — 760
15
wazao wa Binui — 648
16
wazao wa Bebai — 628
17
wazao wa Azgadi — 2,322
18
wazao wa Adonikamu — 667
19
wazao wa Bigwai — 2,067
20
wazao wa Adini — 655
21
wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) — 98
22
wazao wa Hashumu — 328
23
wazao wa Besai — 324
24
wazao wa Harifu — 112
25
wazao wa Gibeoni — 95
26
watu wa Bethlehemu na Netofa — 188
27
watu wa Anathothi — 128
28
watu wa Beth-Azmawethi — 42
29
watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi — 743
30
watu wa Rama na Geba — 621
31
watu wa Mikmashi — 122
32
watu wa Betheli na Ai — 123
33
watu wa Nebo — 52
34
watu wa Elamu — 1,254
35
watu wa Harimu — 320
36
watu wa Yeriko — 345
37
watu wa Lodi, Hadidi na Ono — 721
38
watu wa Senaa — 3,930
39
Makuhani: wazao wa Yedaya (kupitia familia ya Yeshua) — 973
40
wazao wa Imeri — 1,052
41
wazao wa Pashuri — 1,247
42
wazao wa Harimu — 1,017
43
Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia ukoo wa Hodavia) — 74
44
Waimbaji: wazao wa Asafu — 148
45
Mabawabu wa malango: wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai — 138
46
Wanethini wa Hekaluni: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47
Kerosi, Sia, Padoni,
48
Lebana, Hagaba, Shalmai,
49
Hanani, Gideli, Gahari,
50
Reaya, Resini, Nekoda,
51
Gazamu, Uza, Pasea,
52
Besai, Meunimu, Nefusimu,
53
Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54
Basluthi, Mehida, Harsha,
55
Barkosi, Sisera, Tema,
56
Nesia na Hatifa.
57
Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58
Yaala, Darkoni, Gideli,
59
Shefatia, Hatili, Pokereth-Hazebaimu na Amoni.
60
Wanethini wote na wazao wa watumishi wa Solomoni — 392
61
Wafuatao ni watu waliorudi kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamii zao zilitokana na Israeli:
62
wazao waDelaya, Tobia na Nekoda — 642
63
Na kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo.)
64
Hawa walitafuta katika orodha ya jamii zao, lakini hawakuonekana kwa hiyo waliondolewa katika ukuhani kama watu najisi.
65
Kwa hiyo, Tirshatha aliagiza kuwa wasile cho chote miongoni mwa vyakula vitakatifu mpaka atakapopatikana kuhani ahudumuye kwa Urimu na Thumimu.
66
Jumla ya watu wote waliorudi kutoka utumwani uhamishoni walikuwa 42,360;
67
tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwemo waimbaji wanaume na wanawake 245.
68
Walikuwako farasi 736, nyumbu 245
69
ngamia 435 na punda 6,720.
70
Baadhi ya wakuu wa mbari walichangia kazi ya ujenzi. Tirshatha alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50 na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71
Baadhi ya wakuu wa mbari walikabidhi kwenye hazina kwa ajili ya kazi darkoni 20,000 za dhahabu na mane 2,200 za fedha.
72
Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73
Makuhani, Walawi, mabawabu wa malango, waimbaji na Wanethini, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli wengine wote, waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13