bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Numbers 30
Numbers 30
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
1
Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndilo BWANA analoagiza:
2
Wakati mwanaume awekapo nadhiri kwa BWANA, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.
3
“Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwa BWANA, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi,
4
na baba yake akasikia kuhusu nadhiri au ahadi yake lakini asimwambie lo lote, ndipo nadhiri zake zote na kila ahadi aliyoiweka na kujifunga kwayo itathibitika.
5
Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake ye yote aliyojifunga kwayo itakayosimama; BWANA atamwacha huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.
6
“Ikiwa ataolewa baada ya kuweka nadhiri au baada ya midomo yake kutamka ahadi fulani bila kufikiri akawa amejifunga hivyo,
7
na mume wake akasikia habari hiyo asimwambie neno lo lote, ndipo nadhiri zake ama ahadi zake ambazo alikuwa amejifunga nazo zitathibitika.
8
Lakini ikiwa mume wake atamkataza atakaposikia kuhusu hilo, atakuwa ametangua nadhiri ambazo zilikuwa zimemfunga mkewe, ama ahadi aliyotamka pasipo kufikiri ambayo amejifunga kwayo, naye BWANA atamwacha huru yule mwanamke.
9
“Nadhiri yo yote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachika vitakuwa vimemfunga.
10
“Ikiwa mwanamke anayeishi na mumewe ataweka nadhiri ama kujifunga mwenyewe kwa ahadi chini ya kiapo,
11
na mumewe akasikia kuhusu jambo hili lakini asimwambie lo lote wala hakumkataza, ndipo viapo vyake vyote au ahadi zinazomfunga zitakapothibitika.
12
Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zo zote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, na BWANA atamweka huru yule mwanamke.
13
Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri ye yote anayoweka, au ahadi ye yote aliyoweka kwa kuapa ili kujikana mwenyewe.
14
Lakini ikiwa mumewe hasemi lo lote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lo lote kwa mkewe anapoyasikia hayo.
15
Hata hivyo, ikiwa mumewe atavibatilisha baada ya kusikia hayo, basi atawajibika kwa hatia ya mkewe.”
16
Haya ndiyo masharti ambayo BWANA alimpa Mose kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36