bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
/
Romans 11
Romans 11
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
1
Basi nauliza, je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Abrahamu kutoka kabila la Benyamini.
2
Mungu hajawakataa watu wake, ambao yeye aliwajua tangu mwanzo. Je, hamjui yale maandiko yasemayo kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Israeli?
3
Alisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?”
4
Je, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.”
5
Vivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu.
6
Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.
7
Tuseme nini basi? Kile kitu ambacho Israeli alikitafuta kwa bidii hakukipata. Lakini waliochaguliwa walikipata. Waliobaki walifanywa wagumu,
8
kama ilivyoandikwa: “Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo, macho ili wasiweze kuona na masikio ili wasiweze kusikia, hadi leo.”
9
Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe tanzi na mtego wa kuwanasa, kitu cha kuwakwaza waanguke, na adhabu kwao.
10
Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima.”
11
Hivyo nauliza tena, je, Waisraeli walijikwaa ili waanguke na kuangamia kabisa? La, hasha! Lakini kwa sababu ya makosa yao, wokovu umewafikia watu Mataifa, ili kuwafanya Waisraeli waone wivu.
12
Basi ikiwa kujikwaa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
13
Sasa ninasema nanyi watu Mataifa. Maadamu mimi ni mtume kwa watu Mataifa, naitukuza huduma yangu
14
ili kuwafanya watu wangu waone wivu na hivyo kuwaokoa baadhi yao.
15
Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa?
16
Kama sehemu ya donge la unga uliotolewa kuwa limbuko ni mtakatifu, basi unga wote ni mtakatifu, nalo shina kama ni takatifu, vivyo hivyo na matawi nayo.
17
Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka katika shina la mzeituni,
18
basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili. Si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe.
19
Basi utasema, “Matawi yale yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika hilo shina.”
20
Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa.
21
Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, wala hatakuhurumia wewe.
22
Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.
23
Wao nao wasipodumu katika kutokuamini kwao, watapandikizwa tena kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena kwenye hilo shina.
24
Ikiwa wewe ulikatwa kutoka katika kile ambacho kwa asili ni mzeituni mwitu na kupandikizwa kinyume cha asili kwenye mzeituni uliopandwa, si rahisi zaidi matawi haya ya asili kupandikizwa tena kwenye shina lake la mzeituni!
25
Ndugu zangu, ili msije mkajidai kuwa wenye hekima kuliko mlivyo, nataka mfahamu siri hii: Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu Mataifa watakaoingia itimie.
26
Hivyo Israeli wote wataokolewa kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.
27
Hili ndilo Agano langu nao nitakapoziondoa dhambi zao.”
28
Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani,
29
kwa maana akishawapa watu karama haziondoi, wala wito wake.
30
Kama vile ninyi wakati fulani mlivyokuwa waasi kwa Mungu lakini sasa mmepata rehema kwa sababu ya kutokutii kwao,
31
hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi ili kwamba wao nao sasa waweze kupata rehema kwa ajili ya rehema za Mungu kwenu.
32
Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.
33
Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!
34
“Ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?”
35
“Au ni nani aliyempa cho chote ili arudishiwe?”
36
Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16