bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
2 Corinthians 3
2 Corinthians 3
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
1
Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine?
2
Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu.
3
Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Al-Masihi, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mwenyezi Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.
4
Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Al-Masihi.
5
Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.
6
Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima.
7
Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu, hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Musa kwa sababu ya ule utukufu wake ingawa ulikuwa ni wa kufifia,
8
je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?
9
Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi?
10
Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Injili.
11
Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu?
12
Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana.
13
Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.
14
Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Torati inasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa.
15
Hata leo Torati ya Musa inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao.
16
Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana Isa, utaji unaondolewa.
17
Basi Bwana Isa ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Mwenyezi Mungu, hapo pana uhuru.
18
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana Isa, ambaye ndiye Roho.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13