bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
2 John 1
2 John 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
1
Mzee: Kwa bibi mteule na watoto wake, niwapendao katika kweli, wala si mimi tu, bali na wale wote waijuayo kweli:
2
kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itaendelea kukaa nasi milele:
3
Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Isa Al-Masihi, Mwanawe Baba, itakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4
Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza.
5
Sasa, bibi mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake.
6
Hili ndilo pendo, kwamba tuenende sawasawa na amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.
7
Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na anampinga Al-Masihi.
8
Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu.
9
Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Al-Masihi, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia.
10
Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu.
11
Yeyote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.
12
Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.
13
Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1