bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
2 Thessalonians 1
2 Thessalonians 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
1
Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kundi la waumini la Wathesalonike mlio katika Mungu Baba yetu na Bwana Isa Al-Masihi:
2
Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Isa Al-Masihi iwe nanyi.
3
Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.
4
Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.
5
Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mwenyezi Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake.
6
Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi
7
na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Isa atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu.
8
Atawaadhibu wale wasiomjua Mwenyezi Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Isa.
9
Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana Isa na utukufu wa uweza wake,
10
siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
11
Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mwenyezi Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.
12
Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Isa lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Isa Al-Masihi.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3