bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
2 Timothy 3
2 Timothy 3
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
1
Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari.
2
Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mwenyezi Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu,
3
wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema,
4
wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mwenyezi Mungu:
5
wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mwenyezi Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.
6
Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya.
7
Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli.
8
Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.
9
Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.
10
Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu,
11
mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana Isa aliniokoa katika hayo yote.
12
Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Al-Masihi Isa atateswa.
13
Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
14
Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani,
15
na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Al-Masihi Isa.
16
Kila Andiko limevuviwa na Mwenyezi Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,
17
ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4