bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Acts 8
Acts 8
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
1
Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya wafuasi wa Isa Al-Masihi huko Yerusalemu, nao waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria.
2
Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana.
3
Lakini kwa habari ya Sauli, yeye alikuwa analiharibu kundi la waumini, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.
4
Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda.
5
Filipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Al-Masihi.
6
Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema.
7
Pepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele na wengi waliopooza na viwete wakaponywa.
8
Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo.
9
Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu,
10
nao watu wote wakubwa kwa wadogo wakamsikiliza na kumaka, wakisema “Mtu huyu ndiye uweza wa Mungu ujulikanao kama ‘Uweza Mkuu.’ ”
11
Wakamfuata kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake.
12
Lakini watu walipomwamini Filipo alipohubiri habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa wanaume na wanawake.
13
Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona.
14
Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko.
15
Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho wa Mwenyezi Mungu,
16
kwa sababu Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Isa.
17
Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho wa Mwenyezi Mungu.
18
Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho wa Mwenyezi Mungu mitume walipoweka mikono juu yao, akataka kuwapa fedha
19
akisema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apate kupokea Roho wa Mwenyezi Mungu.”
20
Petro akamjibu, “Fedha yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu ulidhani unaweza kununua karama ya Mwenyezi Mungu kwa fedha!
21
Wewe huna sehemu wala fungu katika huduma hii kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
22
Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Mwenyezi Mungu. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.
23
Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.”
24
Ndipo Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Mwenyezi Mungu, ili hayo mliyosema lolote yasinitukie.”
25
Nao walipokwisha kutoa ushuhuda na kuhubiri neno la Bwana Isa, wakarudi Yerusalemu wakihubiri Injili katika vijiji vingi vya Samaria.
26
Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.”
27
Hivyo akaondoka. Akiwa njiani akakutana na towashi wa Kushi, aliyekuwa afisa mkuu, mwenye mamlaka juu ya hazina zote za Kandake, Malkia wa Kushi. Huyu towashi alikuwa amekwenda Yerusalemu ili kuabudu,
28
naye akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya.
29
Roho wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”
30
Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, “Je, unaelewa hayo usomayo?”
31
Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.
32
Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, kama mwana-kondoo anyamazavyo mbele yake yule amkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.
33
Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake? Kwa maana maisha yake yaliondolewa kutoka duniani.”
34
Yule towashi akamuuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?”
35
Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza habari njema za Isa.
36
Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamuuliza Filipo, “Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?” [
37
Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu. ”]
38
Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Wakateremka kwenye maji wote wawili, yule towashi na Filipo, naye Filipo akambatiza.
39
Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Mwenyezi Mungu akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi.
40
Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28