bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Colossians 1
Colossians 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
1
Paulo, mtume wa Al-Masihi Isa, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na Timotheo ndugu yetu:
2
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Al-Masihi, waishio Kolosai: Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.
3
Siku zote tunamshukuru Mwenyezi Mungu, Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, tunapowaombea ninyi,
4
kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Al-Masihi Isa, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:
5
imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili
6
iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mwenyezi Mungu katika kweli yote.
7
Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Al-Masihi kwa ajili yenu,
8
ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho wa Mwenyezi Mungu.
9
Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mwenyezi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.
10
Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana Isa, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu,
11
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
12
mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru.
13
Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa,
14
ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.
15
Yeye ni mfano wa Mwenyezi Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16
Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
17
Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
18
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani jumuiya ya waumini, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote.
19
Kwa kuwa ilimpendeza Mwenyezi Mungu kwamba utimilifu wake wote ukae ndani yake,
20
na kwa njia yake aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake, iliyomwagika msalabani.
21
Hapo kwanza mlikuwa mmetengana na Mwenyezi Mungu, na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mienendo yenu mibaya.
22
Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Al-Masihi kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
23
ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.
24
Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu, na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Al-Masihi kwa ajili ya mwili wake, ambao ni jumuiya ya waumini.
25
Mimi nimekuwa mtumishi wa jumuiya ya waumini kwa wajibu alionipa Mwenyezi Mungu ili kuwaletea ninyi Neno la Mungu kwa ukamilifu:
26
Hii ni siri iliyokuwa imefichika tangu zamani na kwa vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu.
27
Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu wa Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Al-Masihi ndani yenu, tumaini la utukufu.
28
Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Al-Masihi.
29
Kwa ajili ya jambo hili, ninajitaabisha, nikijitahidi kwa kadiri ya nguvu zake ambazo hutenda kazi ndani yangu kwa uweza mwingi.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4