bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Ephesians 2
Ephesians 2
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
1
Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu,
2
ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii.
3
Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine yeyote.
4
Lakini Mwenyezi Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema,
5
hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Al-Masihi Isa, yaani, mmeokolewa kwa neema.
6
Mwenyezi Mungu alitufufua pamoja na Al-Masihi na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Al-Masihi Isa,
7
ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Al-Masihi Isa.
8
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu,
9
si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu.
10
Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mwenyezi Mungu, tulioumbwa katika Al-Masihi Isa, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.
11
Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao hapo awali mlikuwa watu wa Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa “wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “waliotahiriwa” (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu),
12
kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi mkiwa hamna tumaini wala Mwenyezi Mungu duniani.
13
Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mwenyezi Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Al-Masihi.
14
Kwa maana yeye mwenyewe ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa wawili, yaani, Wayahudi na watu wa Mataifa, tuwe wamoja kwa kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui uliokuwa kati yetu,
15
kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri zake na maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya ndani yake mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo akifanya amani,
16
naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mwenyezi Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao.
17
Alikuja na kuhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na pia akahubiri amani kwao waliokuwa karibu.
18
Kwa maana kwa kupitia kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
19
Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu, na pia jamaa wa nyumbani mwake Mwenyezi Mungu.
20
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Al-Masihi Isa mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni.
21
Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Bwana Mwenyezi.
22
Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mwenyezi Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya Roho wake Mtakatifu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6