bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Galatians 3
Galatians 3
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
1
Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Isa Al-Masihi aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa.
2
Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mwenyezi Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia?
3
Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili?
4
Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure!
5
Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
6
Kama vile “Ibrahimu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”
7
Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Ibrahimu.
8
Maandiko yakitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, alitangulia kumtangazia Ibrahimu Injili akisema kwamba, “Kwa kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa.”
9
Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Ibrahimu, mtu wa imani.
10
Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Torati.”
11
Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kushikilia sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.”
12
Lakini sheria haitegemei imani. Kinyume chake, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.”
13
Al-Masihi alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”
14
Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Ibrahimu ipate kuwafikia watu wa Mataifa kwa njia ya Al-Masihi Isa, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.
15
Ndugu zangu, nataka nitoe mfano kutoka maisha ya kila siku. Kama vile hakuna mtu awezaye kutangua au kuongeza kitu katika agano la mtu ambalo limekwisha kuthibitishwa, vivyo hivyo kwa hali kama hii.
16
Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Al-Masihi.
17
Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile.
18
Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Ibrahimu urithi kwa njia ya ahadi.
19
Kwa nini basi iwepo sheria? Torati iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Ibrahimu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Torati iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi.
20
Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.
21
Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria.
22
Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Isa Al-Masihi yapate kupewa wale wanaoamini.
23
Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe.
24
Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Al-Masihi, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani.
25
Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.
26
Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Al-Masihi Isa kwa njia ya imani.
27
Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Al-Masihi, mmemvaa Al-Masihi.
28
Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa.
29
Nanyi mkiwa ni mali ya Al-Masihi, basi ninyi ni wa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ile ahadi.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6