bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Genesis 5
Genesis 5
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 6 →
1
Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.
2
Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”
3
Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.
4
Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
5
Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.
6
Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7
Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
8
Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
9
Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10
Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
11
Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.
12
Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13
Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
14
Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.
15
Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16
Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
17
Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.
18
Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Idrisi.
19
Baada ya kumzaa Idrisi, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
20
Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.
21
Idrisi alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22
Baada ya kumzaa Methusela, Idrisi alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
23
Idrisi aliishi jumla ya miaka 365.
24
Idrisi akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.
25
Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
26
Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
27
Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
28
Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29
Akamwita jina lake Nuhu, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na bwana.”
30
Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
31
Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.
32
Baada ya Nuhu kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50