bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Hebrews 5
Hebrews 5
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
1
Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mwenyezi Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
2
Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka.
3
Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na vivyo hivyo kwa ajili ya dhambi za watu.
4
Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mwenyezi Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa.
5
Pia Al-Masihi hakujitwalia utukufu yeye mwenyewe wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mwenyezi Mungu alimwambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.”
6
Pia mahali pengine asema, “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”
7
Katika siku za maisha ya Isa hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mwenyezi Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu.
8
Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata,
9
na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.
10
Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
11
Tunayo mengi ya kusema kuhusu habari ya ukuhani huu, lakini ni vigumu kuyaeleza, kwa sababu ninyi ni wazito wa kuelewa.
12
Kwa hakika, ingawa mpaka wakati huu ingewapasa kuwa walimu, bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za awali za kweli ya Neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu!
13
Kwa maana yeyote aishiye kwa kunywa maziwa bado yeye ni mtoto mchanga, hana ujuzi katika mafundisho kuhusu neno la haki.
14
Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, ambao kwa kujizoeza wamejifunza kupambanua kati ya mema na mabaya.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13