bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Jonah 2
Jonah 2
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
1
Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba bwana Mwenyezi Mungu wake.
2
Akasema: “Katika shida yangu nalimwita bwana, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu.
3
Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka, mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu.
4
Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako, hata hivyo nitatazama tena kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5
Maji yaliyonimeza yalinitisha, kilindi kilinizunguka; mwani ulijisokota kichwani pangu.
6
Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu.
7
“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, bwana, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu.
8
“Wale watu wanaong’ang’ana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
9
Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea dhabihu. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa bwana.”
10
Basi bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4