bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Luke 4
Luke 4
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 5 →
1
Isa, akiwa amejaa Roho wa Mwenyezi Mungu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu hadi nyikani,
2
mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula chochote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.
3
Ibilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”
4
Isa akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ”
5
Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja.
6
Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka.
7
Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”
8
Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mwenyezi Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”
9
Kisha ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa,
10
kwa maana imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake ili wakulinde;
11
nao watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”
12
Isa akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mwenyezi Mungu wako.’ ”
13
Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Isa mpaka wakati mwingine ufaao.
14
Kisha Isa akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho wa Mwenyezi Mungu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.
15
Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.
16
Isa akaenda Nasiri, alipolelewa, na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome,
17
naye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa:
18
“Roho wa Mwenyezi Mungu yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa,
19
na kutangaza mwaka wa Mwenyezi Mungu uliokubalika.”
20
Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
21
Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.”
22
Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yusufu?”
23
Isa akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”
24
Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe.
25
Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.
26
Hata hivyo Ilya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni.
27
Pia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Al-Yasa, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu.”
28
Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana.
29
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali.
30
Lakini yeye akapita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.
31
Kisha Isa akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilaya, na katika siku ya Sabato akawa anafundisha.
32
Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.
33
Ndani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Naye akapiga kelele kwa nguvu akisema,
34
“Tuache! Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”
35
Basi Isa akamkemea yule pepo mchafu, akisema, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” Yule pepo mchafu akamwangusha yule mtu chini mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru.
36
Watu wote wakashangaa, wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!”
37
Habari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile.
38
Isa akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Basi huko alimkuta mama mkwe wa Simoni akiwa ameshikwa na homa kali, nao wakamwomba Isa amsaidie.
39
Hivyo Isa akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka saa ile ile, naye akaanza kuwahudumia.
40
Jua lilipokuwa linatua, watu wakamletea Isa watu wote waliokuwa na maradhi mbalimbali, naye akaweka mikono yake juu ya kila mgonjwa, naye akawaponya.
41
Pepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu! ” Lakini Isa akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Al-Masihi.
42
Kesho yake, kulipopambazuka, Isa alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke.
43
Lakini yeye akawaambia, “Imenipasa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu katika miji mingine pia, kwa maana kwa kusudi hili nilitumwa.”
44
Naye aliendelea kuhubiri katika masinagogi ya Uyahudi.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24