bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
/
Philemon 1
Philemon 1
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jump to:
Chapter 1
1
Paulo, mfungwa wa Al-Masihi Isa, pamoja na Timotheo ndugu yetu: Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu,
2
kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kundi la waumini lile likutanalo nyumbani mwako:
3
Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mwenyezi Mungu Baba yetu na Bwana Isa Al-Masihi.
4
Siku zote ninamshukuru Mwenyezi Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu,
5
kwa sababu ninasikia juu ya imani yako katika Bwana Isa na upendo wako kwa watakatifu wote.
6
Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Al-Masihi.
7
Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.
8
Hata hivyo, ingawa katika Al-Masihi ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda,
9
lakini ninakuomba kwa upendo, mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Al-Masihi Isa,
10
nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.
11
Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.
12
Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa.
13
Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.
14
Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari.
15
Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima.
16
Si kama mtumwa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana Isa.
17
Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe.
18
Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi.
19
Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako.
20
Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana Isa, uuburudishe moyo wangu katika Al-Masihi.
21
Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.
22
Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu.
23
Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Al-Masihi Isa, anakusalimu.
24
Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu.
25
Neema ya Bwana Isa Al-Masihi iwe pamoja na roho zenu. Amen.
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1