bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
2 Thessalonians 2
2 Thessalonians 2
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
1
Basi, ndugu, tunawasihini, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
2
kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msishtushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa barua inayodhaniwa kuwa ni yetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
3
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4
yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5
Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi niliwaambia hayo?
6
Na sasa lizuialo mnalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inafanya kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hadi atakapoondolewa.
8
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;
9
kuja kwa yule mwasi ni kazi ya Shetani, atumiaye uwezo wote, ishara na ajabu za uongo;
10
na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11
Kwa hiyo Mungu anawaletea upotevu mwingi, wauamini uongo;
12
ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
13
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
14
aliyowaitia ninyi kwa Injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
15
Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa barua yetu.
16
Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,
17
awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3