bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Deuteronomy 11
Deuteronomy 11
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 12 →
1
Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika siku zote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake.
2
Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na watoto wenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyooka,
3
na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri;
4
na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi wao, na magari yao; na alivyowafunika kwa maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandama, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo;
5
na mambo aliyowafanyia ninyi nyikani, hadi mkafika mahali hapa;
6
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
7
lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.
8
Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi mwivukiayo kuimiliki;
9
nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali
10
Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinyunyizia maji kwa mguu wako, kama shamba la mboga;
11
lakini nchi muivukayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyunyizwa maji ya mvua ya mbinguni;
12
nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, yako juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.
13
Tena itakuwa, mtakapoyazingatia kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,
14
ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako.
15
Nami nitakupa nyasi katika mashamba yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.
16
Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu;
17
hasira za BWANA zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo BWANA.
18
Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
19
Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
20
Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako;
21
ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana wenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
22
Kwa kuwa kama mtayazingatia kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye;
23
ndipo BWANA atakapowafukuza mataifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuliko ninyi.
24
Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.
25
Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
26
Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;
27
baraka ni hapo mtakapoyafuata maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;
28
na laana ni hapo msipotii maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkapotoka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
29
Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uiendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.
30
Je! Haiwi ng'ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waishio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More?
31
Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo.
32
Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34