bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Ezra 2
Ezra 2
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 3 →
1
Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;
2
ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli;
3
wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.
4
Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.
5
Wazawa wa Ara, mia saba sabini na watano.
6
Wana wa Pahath-Moabu, wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili.
7
Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
8
Wana wa Zatu, mia tisa arobaini na watano.
9
Wana wa Zakai, mia saba na sitini.
10
Wana wa Binui, mia sita arobaini na wawili.
11
Wana wa Bebai, mia sita ishirini na watatu.
12
Wana wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili.
13
Wazawa wa Adonikamu, mia sita sitini na sita.
14
Wana wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita.
15
Wana wa Adini, mia nne hamsini na wanne.
16
Wana wa Ateri, wana wa Hezekia, tisini na wanane.
17
Wana wa Besai, mia tatu ishirini na watatu.
18
Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.
19
Wana wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu.
20
Watu wa Gibari, tisini na watano.
21
Watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu.
22
Watu wa Netofa, hamsini na sita.
23
Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane.
24
Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili.
25
Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu.
26
Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja.
27
Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili.
28
Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu.
29
Watu wa Nebo, hamsini na wawili.
30
Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita.
31
Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
32
Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini.
33
Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano.
34
Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano.
35
Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini.
36
Makuhani; wana wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu.
37
Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.
38
Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba.
39
Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.
40
Walawi; wana wa Yeshua, wana wa Kadmieli wana wa Hodavia, sabini na wanne.
41
Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane.
42
Akina bawabu; wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa.
43
Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;
44
wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni;
45
wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu;
46
wana wa Hagabu, wana wa Salmai, wana wa Hanani;
47
wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Reaya;
48
wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gazamu;
49
wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai;
50
wana wa Asna, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu;
51
wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri;
52
wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha;
53
wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;
54
wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
55
Wazawa wa watumishi wa Sulemani; wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;
56
wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;
57
wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.
58
Wanethini wote, pamoja na wana wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
59
Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha koo za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;
60
wana wa Delaya, wana wa Tobia na wana wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili.
61
Tena wa makuhani; wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.
62
Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
63
Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
64
Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini,
65
tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.
66
Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arobaini na watano;
67
ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini.
68
Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake;
69
wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani.
70
Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10