bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Genesis 23
Genesis 23
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 24 →
1
Basi umri wake Sara ulikuwa miaka mia moja na ishirini na saba, ndio umri wake Sara.
2
Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akamlilia na kumwombolezea Sara.
3
Akaondoka Abrahamu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na wana wa Hethi, akinena,
4
Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.
5
Wazawa wa Hethi wakamjibu Abrahamu, wakamwambia,
6
Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako.
7
Abrahamu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi.
8
Naye akazungumza nao, akisema, Ikiwa nia yenu nimzike maiti wangu atoke mbele yangu, mnisikie, mkaniombee kwa Efroni mwana wa Sohari,
9
ili kwamba anipe pango la Makpela, iliyo katika mpaka wa shamba lake, na anipe kwa kima kilicho kamili, katikati yenu, iwe milki yangu ya kuzikia.
10
Basi Efroni alikuwa akiketi kati ya wazawa wa Hethi. Efroni Mhiti akamjibu Abrahamu, na wazawa wa Hethi wanasikiliza, hata watu wote waingiao mlango wa mji wake, akisema,
11
Sivyo, bwana wangu, unisikilize. Lile shamba nakupa, na pango lililomo nakupa; mbele ya wana wa watu wangu nakupa, uzike maiti wako.
12
Abrahamu akainama mbele ya watu wa nchi.
13
Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.
14
Efroni akamjibu Abrahamu, akamwambia,
15
Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, ni nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.
16
Abrahamu akakubali maneno ya Efroni. Abrahamu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
17
Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango lililokuwemo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa
18
kuwa mali yake Abrahamu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.
19
Basi baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
20
Na lile shamba, na pango lililomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Abrahamu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50