bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Joshua 19
Joshua 19
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 20 →
1
Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.
2
Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, Sheba, Molada;
3
Hasar-shuali, Bala, Esemu;
4
Eltoladi, Bethuli, Horma;
5
Siklagi, Beth-markabothi, Hasarsusa;
6
Bethlebaothi na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;
7
Aini, Rimoni, Etheri na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;
8
tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kotekote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila la wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.
9
Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.
10
Kisha sehemu ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikia hadi Saridi;
11
kisha mpaka wao ukakwea ukaendelea upande wa magharibi, hadi kufikia Marala, nao ukafikia hadi Dabeshethi; nao ukafikia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu;
12
kisha ukazunguka kutoka Saridi kuendelea upande wa mashariki kwa kuelekea mawio ya jua hata kufikia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea ukaendelea Yafia;
13
kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hadi kufikia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikialo hadi Nea;
14
kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hadi Hanathoni; kisha mwisho wake ulikuwa katika bonde la Iftaeli;
15
Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
16
Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
17
Kisha sehemu ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, na ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao.
18
Na mpaka wao ulifikia Yezreeli, Kesulothi, Shunemu;
19
Hafaraimu, Shioni, Anaharathi;
20
Rabithu, Kishioni, Ebesi;
21
Remethi, Enganimu, Enhada, Bethpasesi;
22
na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
24
Kisha sehemu ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao.
25
Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu;
26
Alameleki, Amadi na Mishali; nao ukafika hadi Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikia hadi Shihor-libnathi;
27
kisha ukazunguka kuelekea mawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikia hadi Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hadi Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hadi Kabuli upande wa kushoto;
28
na Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana, hadi kufikia Sidoni Kuu;
29
kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;
30
na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
32
Kisha sehemu ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao.
33
Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabneeli, hadi kufikia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani;
34
tena mpaka ulizunguka kuendelea upande wa magharibi hadi Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikia hadi Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikia hadi Asheri upande wa magharibi, tena ulifikia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea mawio ya jua.
35
Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi;
36
Adama, Rama Hazori;
37
Kedeshi, Edrei, Enhasori;
38
Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
39
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
40
Kisha sehemu ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao.
41
Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, Eshtaoli, Irishemeshi;
42
Shaalabini, Aiyaloni, Ithla;
43
Eloni, Timna, Ekroni;
44
Elteka, Gibethoni, Baalathi;
45
Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni;
46
Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa.
47
Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.
48
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
49
Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;
50
kulingana na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.
51
Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele za BWANA, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24