bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Leviticus 21
Leviticus 21
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 22 →
1
Kisha BWANA akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;
2
isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume;
3
na kwa ajili ya dada yake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mwanamume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo.
4
Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi.
5
Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao.
6
Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.
7
Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.
8
Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi BWANA niwatakasaye ninyi, ni mtakatifu.
9
Na binti wa kuhani yeyote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa hadi afe.
10
Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;
11
wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;
12
wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake uko juu yake; mimi ndimi BWANA.
13
Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.
14
Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
15
Naye asiwatie unajisi wazawa wake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.
16
Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
17
Nena na Haruni, umwambie, Mtu yeyote wa vizazi vyenu vyote aliye na kilema asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.
18
Kwa kuwa mtu aliye na kasoro ya kimwili hatakaribia, asiyeona, aliyelemaa mguu au mtu aliyejeruhika uso, au kiungo kilichozidi kiupasavyo mwili,
19
au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,
20
au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye uvimbe, au aliyevunjika mapumbu;
21
mtu yeyote wa uzao wa Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
22
Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.
23
Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.
24
Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27