bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
/
Song of Solomon 5
Song of Solomon 5
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 6 →
1
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bibi harusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
2
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
3
Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimenawa miguu; niichafueje?
4
Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukasisimuka kwa ajili yake.
5
Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondosha manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.
6
Nilimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
7
Walinzi wazungukao mjini waliniona, Wakanipiga na kunitia jeraha, Walinzi walindao kuta zake Wakaninyang'anya shela yangu.
8
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.
9
Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Wewe uliye mzuri katika wanawake, Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Hata wewe utusihi hivyo?
10
Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;
11
Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru;
12
Macho yake ni kama hua penye vijito, Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa;
13
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondosha matone ya manemane;
14
Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;
15
Miguu yake ni kama nguzo za marimari, Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu; Sura yake ni kama Lebanoni, Ni bora mfano wa mierezi;
16
Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana kwa ujumla. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8