bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 John 1
2 John 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
1
Mimi mzee nakuandikia wewe, mke mkuu uliyechaguliwa, hata watoto wako, ninaowapenda kweli. Lakini si mimi tu ninayewapenda kweli, ila hata wote waliyoyatambua yaliyo ya kweli.
2
Tunawapenda kwa ajili ya kweli ikaayo mwetu, nasi tutakuwa nayo kale na kale.
3
Upole na huruma na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo aliye mwana wa Baba utukalie, tupendane kweli!
4
Nalifurahi sana kwa kuona, wengine walio watoto wako wanavyoishika njia ya kweli, kama tulivyoagizwa na Baba.
5
Hata sasa nakuomba, mke mkuu tupendane; si kama nitakuandikia agizo jipya, ni lilelile, tulilokuwa nalo tangu mwanzo.
6
Nako kupendana ni huko, tukifanya mwenendo, kama alivyotuagiza. Hilo ndilo agizo lake, kama mlivyosikia tangu mwanzo, mwendelee na kulifuata.
7
Kwani wapotevu wengi wametokea ulimwenguni wasioungama kwamba: Yesu Kristo amekuja mwenye mwili wa kimtu. Aliye hivyo ni mpotevu na mpinga Kristo.
8
Jiangalieni, msiyapoteze mapato ya kazi zenu, ila mpewe mshahara wote!
9
Kila anayesogeza mpaka, asikae penye mafundisho ya Kristo, hanaye Mungu; anayekaa penye mafundisho huyu anaye Baba hata Mwana.
10
Mtu akija kwenu asiyeyaleta mafundisho haya, msimpokee nyumbani mwenu, wala salamu msimpe!
11
Kwani mwenye kumsalimia huwa mwenziwe wa kazi zake mbaya.
12
Ninayo mengi ya kuwaandikia ninyi, lakini sikutaka kuyamaliza kwa karatasi na wino, ila nangojea kwamba: Nitakuja kwenu na kusema nanyi kinywa kwa kinywa, furaha yetu itimie.
13
Watoto na dada yako aliyechaguliwa naye wanakusalimu. Amin.
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1