bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Peter 3
2 Peter 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Wapendwa, barua hii ni ya pili, ninayowaandikia ninyi. Nami katika zote mbili nayakeshesha mawazo yenu yaliyo ya kweli kwa kuwakumbusha:
2
yakumbukeni maneno yaliyosemwa kale na wafumbuaji watakatifu! Tena mlikumbuke nalo agizo la Bwana na mwokozi, mliloambiwa na mitume wenu!
3
*Kwanza litambueni neno hili: siku za mwisho patatokea wafyozaji wenye mafyozi mabaya wanaoendelea na kuzifuata tamaa zao wenyewe
4
wakisema: Kiagio cha kurudi kwake kiko wapi? Kwani tangu hapo, baba zetu walipolala, vyote viko vivyo hivyo, kama vilivyokuwa mwanzoni vilipoumbwa.
5
Nao walio hivyo hawataki kuliona neno hili: mbingu zilikuwako toka kale, nayo nchi ilikuwa imetoka majini kwa neno la Mungu ilishikizika mlemle majini.
6
Kisha ule ulimwengu wa kale uliangamia, ulipofurikiwa na maji.
7
Nazo mbingu za sasa pamoja na nchi zikalimbikwa kwa neno lilelile, zikawekwa, ziteketezwe na moto siku ile, watu wasiomcha Mungu watakapohukumiwa, waangamie.
8
Lakini wapendwa, neno hili moja msilisahau: Kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, nayo miaka elfu ni kama siku moja!
9
Bwana hakawii kukitimiza kiagio, kama wengine wanavyowaza kwamba: Hukawia. Ila huwavumilia ninyi, kwani hataki, wengine waangamie, ila anataka, wote wageuke na kujuta.
10
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; ndipo, mbingu zitakapotoweka kwa shindo kuu, nayo yaliyoko tangu mwanzo yatayeyuka kwa kuchomwa na moto, hata nchi za kazi zilizomo zitateketezwa.
11
Hizi zote zikienda kuyeyuka hivyo, je? Haiwapasi kuutakasa mwenendo wenu kwa kumcha Mungu?
12
Kisha mwingoje siku ya Bwana, itakapokutia, mpate kumkimbilia, mbingu zitakapoyeyuka kwa kuunguzwa na moto, yaliyoko tangu mwanzo yatakapoteketea kwa kuchomwa na moto!
13
Lakini twatazamia mbingu mpya na nchi mpya zitakazokaa wongofu, kama tulivyoagiwa naye.
14
Kwa hiyo, wapendwa, mkiyatazamia hayo jikazeni, mpate kuonekana kuwa wenye utengemano pasipo kilema wala pasipo doadoa!*
15
Tena uvumilivu wa Bwana wetu mwuwazie kuwa wokovu, kama naye ndugu yetu mpendwa Paulo alivyowaandikia ninyi kwa ujuzi wake, aliopewa.
16
Ndivyo, anavyoandika katika barua zote akiyasema mambo hayo; lakini mle baruani mwake yamo maneno mengine yaliyo magumu ya kuyajua maana. Nao wasiofundishwa vema nao wasiomtegemea Mungu vema huyapindua, kama wanavyoyapindua hata Maandiko mengine; ndivyo, wanavyojiangamiza wenyewe.
17
Basi, ninyi wapendwa mlioanza kuyatambua hayo, jiangalieni, nanyi msipotezwe na upotevu wao wasioonyeka, mkaanguka na kuiacha ngome yenu wenyewe!
18
Ila endeleeni kukuwa mkigawiwa mema, tena mkimtambua Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo! Yeye atukuzwe sasa mpaka siku isiyo na mwisho! Amin.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3