bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
2 Thessalonians 3
2 Thessalonians 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
1
Kisha, ndugu, mtuombee sisi kwa Mungu, Neno la Bwana liendelee na kutukuzwa vivyo hivyo kama kwenu!
2
Tena tuombeeni, tuokolewe mikononi mwa watu walio wapuzi na wabaya! Kwani sio wote wawezao kumtegemea Bwana.
3
Lakini Bwana ni mwelekevu atakayewashupaza na kuwalinda, yule Mbaya asiwajie.
4
Kwa ajili yenu tunamtumaini Bwana kwamba: Tunayowaagiza, mwayashika sasa, hata siku za nyuma mtayashika.
5
Bwana aiongoze mioyo yenu, iufikie upendo wa Mungu na uvumilivu wa Kristo!
6
*Ndugu, tunawaagiza ninyi, kwa nguvu ya Jina la Bwana Yesu Kristo, mtengane na kila ndugu anayeendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, asiufuate ufundisho, mlioupata kwetu sisi.
7
Kwani mwajua wenyewe, jinsi inavyowapasa kutuiga, kwa sababu hatukukaa kwenu kiovyoovyo tu.
8
Hakuna, ambaye tulikula chakula chake bure, ila tulijisumbua na kujiumiza tukifanya kazi usiku na mchana kwa kukataa kumlemea mtu ye yote wa kwenu.
9
Hatukuvifanya hivyo kwamba: Hatu wakuu, ila tulitaka kuwapa ninyi vielezo, mpate kutuiga.
10
Kwani tulipokuwa kwenu tuliwaagiza hata neno hili: Mtu asiyetaka kufanya kazi asipate chakula!
11
Kwani twasikia: Kwenu wako wanaoendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, hawafanyi kazi, ila hufanya mapuzi.
12
Walio hivyo tunawaagiza na kuwaonya machoni pake Bwana Yesu Kristo, watulie, wapate kufanya kazi na kula chakula chao wenyewe.
13
Lakini ninyi, ndugu, msichoke kufanya yaliyo mazuri!*
14
Lakini mtu asipoyatii maneno yetu yaliyomo humu baruani, huyo mjulisheni mkikataa kuchanganika naye, apatwe na soni!
15
Lakini msimwazie kuwa mchukivu, ila mwonyeni kindugu!
16
Lakini yeye Bwana aliye mwenye utangemano awape kutengemana po pote katika mambo yote! Bwana awe nanyi nyote!
17
Salamu hii naiandika kwa mkono wangu mimi Paulo; huu ndio mwandiko wangu katika barua zote. Hivi ndivyo, ninavyoandika.
18
Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie ninyi nyote! Amin.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
All chapters:
1
2
3