bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
3 John 1
3 John 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
1
Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, mpendwa wangu, ninayempenda kweli.
2
Mpendwa, kuliko yote nakuombea, ukae vema na kuwa mzima, kama roho yako inavyokaa vema.
3
Kwani nalifurahi sana, ndugu walipokuja na kutushuhudia, kuwa u mwenye kweli, kama wewe unavyoishika njia ya kweli.
4
Hakuna linalonifurahisha kuliko lile la kusikia, ya kuwa watoto wangu huishika njia ya kweli.
5
Mpendwa, u mwelekevu katika yote, unayowafanyia ndugu walio wageni.
6
Nao walikushuhudia mbele ya wateule, unavyowapenda. Kwa hiyo utafanya vizuri utakapowasindikiza, kama inavyowapasa walioko mbele ya Mungu.
7
Kwani walitoka kulitangaza Jina lake tu, hawataki kupewa cho chote kwa watu wa kimizimu.
8
Nasi imetupasa kuwapokea watu kama hao, tusaidiane kufanya kazi za kweli.
9
Yako mengine, niliyoyaandikia wateule. Lakini Diotirefe anayependa kuwa mkubwa wao hatusikii sisi.
10
Kwa hiyo nitakapokuja nitazikumbusha kazi zake, anazozifanya akituteta sisi kwa maneno mabaya. Nayo hayo hayamtoshi: mwenyewe hawapokei ndugu, nao wanaotaka kuwapokea huwazuia, kisha huwafukuza kwenye wateule.
11
Mpendwa, usiuige uovu, ila uuige wema! Anayefanya yaliyo mema ni wa Kimungu; anayefanya yaliyo maovu hakumwona Mungu.
12
Lakini Demetirio hushuhudiwa nao wote, naye hushuhudiwa kweli. Hata sisi twamshuhudia, nawe wajua, ya kuwa ushahidi wetu ni wa kweli.
13
Nalikuwa nayo mengi ya kukuandikia, lakini sitaki kukuandikia tu kwa wino na kalamu,
14
ila nangojea, nikuone upesi, tusemeane kinywa kwa kinywa.
15
Utengemano ukukalie! Wapenzi wanakusalimu. Nisalimie wapenzi kila kwa jina lake!
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1