bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Jonah 2
Jonah 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
1
Bwana akaagiza samaki mkubwa, aje ammeze Yona, Yona akawamo tumboni mwa samaki huyo siku tatu mchana na usiku.
2
Mle tumboni mwa huyo samaki Yona akamwomba Bwana Mungu wake
3
kwamba: Nimemlilia Bwana niliposongeka, akaniitikia; kuzimuni ndani nimemlalamikia, aniokoe, ndipo, alipoisikia sauti yangu.
4
Umenitupa vilindini baharini ndani, mafuriko ya maji yanizunguke, mawimbi yako yote na maumuko yako yote yakapita juu yangu.
5
Nami nikawaza kwamba: Nimetupwa, nisitokee tena machoni pako, nitawezaje kuliona tena Jumba lako takatifu?
6
Maji yamenizunguka ya kuitosa nayo roho yangu, vilindi vimenizunguka, majani ya baharini yamekizinga kichwa changu.
7
Nimezama kuifikia misingi ya milima, makomeo ya nchi yamenifungia kale na kale, lakini wewe Bwana Mungu wangu umenitoa kuzimuni, niwe mzima.
8
Roho yangu ilipokuwa katika kuzimia ndani yangu, ndipo, nilipomkumbuka Bwana, maombo yangu yakakufikia katika Jumba lako takatifu.
9
Washikao mizimu iliyo ya uwongo tu humwacha awahurumiaye,
10
lakini mimi nitapaza sauti za kukushukuru, ziwe ng'ombe zangu za tambiko, nitakazokutolea, nayo, niliyokuapia na niyalipe! Wokovu uko kwake Bwana.
11
Ndipo, Bwana alipomwagiza yule samaki, naye akaja kumtapika Yona pwani.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4