bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Obadiah 1
Obadiah 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
1
Ndivyo, Bwana Mungu anavyosema kwa ajili ya Edomu: Tumesikia mbiu kwake Bwana, ya kuwa mjumbe ametumwa kwenda kwa mataifa kwamba: Ondokeni! Na tuondoke kwenda kupigana naye!
2
Utaniona, nikikufanya kuwa mdogo katika mataifa, ubezwe kabisa wewe!
3
Majivuno ya moyo wako yamekudanganya ukaaye nyufani kwenye miamba katika makao yaliyoko huko juu, ukasema moyoni mwako: Yuko nani atakayenibwaga chini?
4
Lakini ijapo uvijenge vituo vyako juu kabisa kama tai, ijapo utue katikati ya nyota, huko nako nitakubwaga chini; ndivyo, asemavyo Bwana.
5
Kama wezi wangekujia, au kama waangamizaji wangekujia usiku, wasingeiba tu, mpaka wakitoshewa? Lakini nawe ungekuwa umeangamizwa kabisa. Kama wachuma zabibu wangekujia,
6
Lakini tazameni, mali za Esau zilivyotafutwa zote, malimbiko yake nayo yalivyochunguzwa!
7
Wote, uliofanya maagano nao, wamekukimbiza hata mipakani; wote, uliopatana nao, wamekudanganya, wakakushinda, waliokula chakula chako wamekutegea matanzi chini, lakini mwenyewe huyatambui maana.
8
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku hiyo, nitakapowapoteza werevu wa kweli kwake Edomu, sipo, utambuzi nao utakapopotea milimani kwa Esau?
9
Ndipo, mafundi wenu wa vita, ninyi Watemani, watakapokata tamaa, kusudi kila mmoja ang'olewe milimani kwa Esau kwa kuuawa.
10
Kwa hivyo, ulivyomkorofisha ndugu yako Yakobo, soni zitakufunika, mpaka uangamie kale na kale.
11
Kwani walisimama upande mwingine siku ile, wengine walipoziteka mali zake, wageni walipoingia malangoni mwake na kuupigia Yerusalemu kura, ndipo, wewe nawe ulipokuwa kama mwenzao wao hao.
12
Lakini usimwonee ndugu yako, akipatwa na siku mbaya, siku ikiwa ya kuona mambo mageni! Wala usiwafurahie wana wa Yuda siku, wakiangamia! Wala usiwe na madomo makubwa siku, wakisongeka!
13
Wala usiingie malangoni mwao walio ukoo wangu siku, wakiteseka! Wala usiwaonee nawe, wakipatwa na mabaya siku, wakiteseka! Wala usiinyoshe mikono yako kukamata mali zao siku, wakiteseka!
14
Wala usisimame penye njia panda kuwaua watu wao waliokimbia! Wala masao yao usiwatie mikononi mwa adui siku, wakisongeka!
15
Kwani siku ya Bwana iko karibu, iwajie wao wa mataifa yote; ndipo, utakapofanyiziwa, kama ulivyofanya, matendo yako yakikurudia kichwani pako.
16
Kwani kama ulivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu, ndivyo, mataifa yote watakavyokunywa pasipo kukoma, watakunywa na kumeza vibaya, wawe kama watu wasiokuwapo kabisa.
17
Lakini mlimani pa Sioni watakuwapo waliojiponya, napo patakuwa Patakatifu.
18
Nao walio mlango wa Yakobo watakuwa moto, nao walio mlango wa Yosefu watakuwa miali ya moto, lakini walio wa mlango wa Esau watakuwa majani makavu, ndiyo watakayoyawasha na kuyala. Kwa hiyo hawatakuwapo walio masao ya Esau, kwani Bwana ameyasema.
19
Nao wakaao upande wa kusini wataitwaa milima ya Esau, nao wakaao mrimani wataitwaa nchi ya Wafilisti, nayo mashamba ya Efuraimu nayo mashamba ya Samaria watayatwaa, nao Wabenyamini watatwaa Gileadi.
20
Navyo vikosi vya wana wa Isiraeli waliotekwa na kuhamishwa ndio watakaoitwaa nchi ya Kanaani mpaka Sareputa, nao Wayerusalemu waliotekwa na kuhamishwa Sefaradi wataitwaa miji iliyoko upande wa kusini.
21
Kisha waokozi wataupanda mlima wa Sioni, waipatilize milima ya Esau; lakini ufalme utakuwa wake Bwana.
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1