bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Philippians 2
Philippians 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
1
Hivyo mlivyo naye Kristo, nawabembeleza kwamba: Ikiwa mwatulizana mioyo kwa kupendana, ikiwa m wenye roho moja, au ikiwa m wenye mioyo ya kuoneana uchungu na huruma,
2
ikiwa hivyo, itimilizeni furaha yangu, mawazo yenu yakiwa yayo hayo ya kupendana kila mtu na mwenziwe, mioyo ikiwa mmoja tu wa kulitaka neno lili hili la kwamba:
3
Pasifanyike jambo lolote kwa kuchokozana wala kwa kujitakia majivuno ya bure, ila mnyenyekeane kila mtu akimwazia mwenziwe kuwa mkubwa kuliko yeye!
4
Kila mtu asiyaangalie yaliyo yake tu, ila na ayaangalie nayo yaliyo yake mwenziwe!*
5
*Mioyoni mwenu myawaze yaleyale, Kristo Yesu aliyoyawaza!
6
Yeye alikuwa mwenye sura yake Mungu, tena kule kufanana naye Mungu hakushikamana nako kama ni kitu, alichokiponyoka.
7
Ila alijivua mwenyewe sura ya Kimungu, akajivika sura ya kitumwa, akawa amefanana na watu; walipomtazama, akaonekana, kuwa kama mtu mwenyewe.
8
Akajinyenyekeza mwenyewe, akawa mwenye kutii mpaka kufa, kweli mpaka kufa msalabani.
9
Kwa hiyo naye Mungu alimkweza mbinguni, akampatia Jina lililo kuu kuliko majina yote,
10
maana katika Jina lake Yesu wote wapige magoti, wao walioko mbinguni nao waliopo nchini nao walioko kuzimuni,
11
kila ulimi uungame kwamba: BWANA ni YESU KRISTO; hivyo ndivyo, naye Mungu Baba atakavyotukuzwa.*
12
Wapenzi wangu, kama mlivonitii siku zote, ikiwa niko kwenu, hata ikiwa siko kama siku hizi za sasa: Usumbukieni wokovu wenu wenyewe mkitetemeka kwa kuogopa!
13
Kwani Mungu ndiye aliyewapa kwanza mioyo ya kutaka, kisha ndiye atakaye wapa nako kuyamaliza yampendezayo.
14
Yote yafanyeni pasipo kunung'unika na pasipo kuwaza mengi,
15
mtu asione la kuwaonya, mkiwa wenye hilo Neno moja tu! Hivyo mtakuwa wana wa Mungu wakaao pasipo kilema katikati yao wa ukoo huu wenye uangamizi na upotovu. Katikati yao ndiko, mnakoangaza, kama mianga inavyoangaza ulimwenguni,
16
mkilishika Neno la uzima; hivyo nami nitapata majivuno siku ya Kristo kwamba: Sikupiga mbio bure, wala sikusumbuka bure.
17
Lakini hata nikiuawa kama ng'ombe ya tambiko, ikiwa ya kuwatumikia tu, nafurahi na kuwafurahisha nanyi nyote.
18
Vivi hivi hata ninyi furahini na kunifurahisha nami!
19
Namngojea Bwana Yesu, aitikie, nimtume Timoteo upesi kwenu, moyo wangu upate kutulia ukitambua, mambo yenu yalivyo.
20
Kwani sinaye mtu mwingine, tuliyepatana naye mioyo kama huyu; naye huyasumbukia kweli mambo yenu.
21
Kwani wote huyafuata yaliyo yao; hawayafuati yaliyo yake Kristo Yesu.
22
Lakini yeye mmemtambua, ya kuwa ni mwelekevu, kwani kama mtoto anavyomtumikia baba yake, vivyo hivyo ameitumikia kazi ya kuutangaza Utume mwema pamoja nami.
23
Nangojea, nipate kumtuma yeye; itakuwa papo hapo, nitakapoona, mambo yangu yatakavyotimilika.
24
Hili nalo nalishika moyoni kwamba: Bwana atanipa nami kuja upesi kwenu.
25
Lakini nalishurutishwa moyoni kumtuma Epafurodito kwenu; yeye ni ndugu na mwenzangu wa kazi na wa vita; kisha ni mtume wenu anayenipatia yenye kunitunza.
26
Akawa akiwatunukia ninyi nyote, akasikitika sana, kwa sababu mlikuwa mmesikia, ya kuwa aliugua.
27
Naye alikuwa mgonjwa kweli, kufa kukamfikia. Lakini Mungu akamhurumia, tena siye yeye tu, ila mimi nami, masikitiko yasifuatane kwangu mimi.
28
Kwa hiyo nimemtuma upesiupesi, mpate kuonana naye na kufurahi tena, nami masikitiko yanipungukie.
29
Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana kwa furaha yote! Nao walio hivyo wapeni macheo!
30
Kwani kwa ajili ya kazi ya Kristo alijifikisha kufani, asijitunzie mwenyewe, akitaka kunifanyizia kazi zote za utumishi, ambazo hamkuweza kunifanyizia.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4