bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
1 John 1
1 John 1
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,
2
(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3
tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
4
Na haya twawaandikieni, illi furaha yenu itimizwe.
5
Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake.
6
Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
7
bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.
8
Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu.
9
Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.
10
Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5