bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
1 Thessalonians 1
1 Thessalonians 1
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
1
PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
2
Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu;
3
wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;
4
tukijua, ndugu mnaopendwa na Mungu, uteule wenu,
5
kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
6
Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,
7
hatta mkawa mfano kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.
8
Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote.
9
Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,
10
na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5