bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
2 John 1
2 John 1
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jump to:
Chapter 1
1
MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;
2
kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hatta milele.
3
Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4
Nalifurahi mno kwa kuwa naliwaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
5
Na sasa, Bibi, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
6
Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Illi ndiyo ile amri, kama ulivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
7
Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.
8
Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.
9
Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.
10
Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11
Maana ampae salamu azishirika kazi zake mbovu.
12
Kwa kuwa nina maneno mengi ya kuwa-andikia, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraja kuja kwenu, na kusema nanyi mdo-mo kwa mdomo, illi furaha yenu itimizwe.
13
Wa-toto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.
Jump to:
Chapter 1
All chapters:
1