bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
/
Matthew 13
Matthew 13
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
1
SIKU ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.
2
Wakamkusanyikia watu wengi, hatta akapanda chomboni, akaketi; na mkutano wote wakasimama pwani.
3
Akasema nao mengi kwa mifano, akinena, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu.
4
Hatta alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila:
5
nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa udongo mwingi: marra zikaota, kwa kuwa na udongo haba;
6
na jua lilipozuka zikanyauka; na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka.
7
Nyingine zikaanguka penye miiba; miiba ikamea, ikazisonga:
8
nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikazaa, hizi mia, hizi sittini, hizi thelathini.
9
Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
10
Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
11
Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.
12
Kwa maana ye yote aliye na mali atapewa, na hado atazidishiwa tele: lakini ye yote asiye nayo, hatta ile aliyo nayo ataondolewa.
13
Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawatazami na wakisikia hawasikii, wala hawafahamu.
14
Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likinena, Kusikia mtasikia, wala hamtafahamu; Mkitazama mtatazama, wala hamtaona:
15
Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao Wakasikia kwa masikio yao, Wakafahama kwa mioyo yao, Wakaongoka, Nikawaponya.
16
Lakini ya kheri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.
17
Kwa maana amin, nawaambieni, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasivaone; na kuyasikia mnayoyasikia, wasiyasikie.
18
Bassi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
19
Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.
20
Nae aliyepandwa penye miamba, huyu ndiye alisikiae lile neno, akalipokea marra kwa furaha;
21
lakini hana mizizi udani yake, hukaa muda mchache; ikitukia shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa.
22
Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.
23
Nae aliyepandwa penye udongo mwema, huyu ndive alisikiae lile neno, na kulifahamu; yeye ndiye azaae matunda, huyu mia, na huyu sittini, na huyu thelathini.
24
Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake:
25
lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake.
26
Baadae majani ya nganu yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27
Watumishi wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? limepatapi bassi magugu?
28
Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumishi wakamwambia, Bassi, wataka twende tukayakusanye?
29
Akasema, La; labuda wakati wa kukusanya magugu, mtangʼoa na nganu pamoja nayo.
30
Viacheni vyote vikue hatta wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno nitawaambia wavimao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita, mkayachome; bali nganu ikusauyeni ghalani mwangu.
31
Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake;
32
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, ni kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hatta ndege za anga huja na kutua katika matawi yake.
33
Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.
34
Haya yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; na pasipo mfano hakuwaambia neno:
35
illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema, Nitafunua kinywa changu kwa mifano, Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
36
Kisha Yesu akawaacha makutano, akaingia nyumbani: wanafunzi wake wakamwendea, wakinena, Tufafanulie mfano wa magugu ya konde.
37
Akajibu, akasema, Azipandiie zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;
38
na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;
39
na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.
40
Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii.
41
Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya katika ufalme wake machukizo yote, nao watendao maasi,
42
na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.
43
Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.
44
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyostirika katika shamba; mtu akaiona, akaificha; na kwa furaha yake akaenda akanza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
45
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mfanya biashara, afafutae lulu nzuri:
46
nae alipoona lulu moja ya thamani kubwa, akaenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.
47
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya za killa namna:
48
hatta lilipojaa, wakalipandisha pwani; wakaketi, wakakusanya zilizo njema vyomboni, bali zilizo mbaya wakazitupa.
49
Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu na wenye haki,
50
na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.
51
Yesu aliwaambia, Mmeyafahamu haya yote? Wakamwambia, Naam, Bwana.
52
Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.
53
Ikawa Yesu alipomaliza mifano hii, akatoka, akaenda zake.
54
Na alipofika inchi yake, akawafundisha katika sunagogi yao, hatta wakashangaa, wakanena, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
55
Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda?
56
na maumbu yake, wote hawako kwetu? Bassi huyu amepata wapi haya yote?
57
Wakachukizwa nae. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika inchi yake mwenyewe, na nyumbani mwake mwenyewe.
58
Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28